Viongozi waonya dhidi ya uchimbaji wa madíni ya baharini

Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Bahari ulioanza jana mjini Nice kusini mwa Ufaransa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema sio busara hata kidogo kuanzisha shughuli za kiuchumi ambazo zitaharibu sehemu ya chini ya bahari na kuathiri viumbehai. Amesema ni jambo la lazima kwa jumuiya ya kimataifa kusitisha uchimbaji wa madini ya baharini.

Idadi ya nchi zinazopinga shughuli hiyo iliongezeka jana Jumatatu hadi 36. Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alitoa wito ya hatua ya wazi kutoka kwa mamlaka ya bahari ili kukomesha “mbio zinazoshuhudiwa” za madini ya baharini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema anaunga mkono mapendekezo hayo na kuhimiza tahadhari wakati nchi zikiendelea kulishughulikia suala hilo jipya la uchimbaji wa madini ya baharini. Wawakilishi wa nchi 130 wanahudhuria mkutano huo wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ulinzi wa bahari utakaokamalizika Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *