Viongozi wahaha kutafuta saini

Viongozi wa timu zinazoshiriki ligi  ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), walikuwa wakipigana vikumbo kusaka saini  za wachezaji wapya katika ,  wakati wa mashindano ya Ramadhani Star Ligi.

Wachezaji  walionekana kuwa na wakati mgumu ni wachezaji wa Miyasi, Marcus Tshi, Emanuel Mulumba na Dan Mwendela  raia wa Congo.

Mwanasposti ililokuwepo uwanjani hapo. lilishuhudia viongozi hao wakiwashawishi  wachezaji hao wajiunge na timu zao.

Mmoja wachezaji hao, Mulumba alikiri kufuatwa ingawa hajataja majina ya viongozi hao; “Ni kweli nimefuatwa kuombwa na viongozi wanne nijiunge na timu zao.”

Jordan Jordan wa Mchenga Star anayecheza namba 4  ‘Power Forward’ alisema hajapata ofa yoyote hadi sasa na itakayokuja na nzuri atajiunga nayo.

“Timu itakayonihitaji  na ofa nzuri nitajiunga kuchezea nayo msimu huu,” alisema Jordan.

Kocha wa mchezo huo kutoka Temeke, John Petar alisema ligi ya msimu huu itakuwa ngumu na timu ambayo haina fedha za kujiendeshea itashindwa kusajili nyota wakali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *