Viongozi kutoka nchi za EAC na SADC kukutana tena kujadili hali ya DRC

Viongozi toka jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, hivi leo watakutana kwa mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kujaribu kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo wa mashariki mwa nchi ya DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kitakachofanyika chini ya uenyekiti wa nchi ya Zimbabwe, kinalenga kujadili hatua zilizofikiwa tangu kikao cha juma lililopita ambapo wakuu wa nchi za SADC waliagiza kuondolewa kwa wanajeshi wao mashariki mwa Congo.

Aidha, viongozi wa jumuiya hizi mbili, walikubaliana kutumia njia ya mazungumzo ya kisiasa kutafuta ufumbuzi wa mzozo unaoendelea, wakati huu waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda wakikalia mji wa Goma na Bukavu.

Rais wa Zimbabwe wakati akizungumza katika mkutano wa awali wa viongozi wa SADC na EAC kuhusu hali ya DRC.
Rais wa Zimbabwe wakati akizungumza katika mkutano wa awali wa viongozi wa SADC na EAC kuhusu hali ya DRC. © Ikulu ya Tanzania

Kikao cha SADC na EAC kinaenda kufanyika wakati hapo kesho rais wa Angola, Joao Lourenco, atakuwa mwenyeji wa wawakilishi wa Serikali ya Kinshasa na wale wa kundi la M23, ambapo watakutana kwa mara ya Kwanza ana kwa ana kujaribu kumaliza tofauti zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *