Viongozi kutoka mataifa wanachama wa SADC na EAC kujadili hali ya DRC

Wakuu wa nchi toka jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya maendeleo ya kusini mwa Afrika, SADC, watakutana hivi leo kwa njia ya mtandao, kujadiliana kuhusu hali inayoendelea mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kitakuwa ni cha pili cha viongozi wa juu tka kwenye jumuiya hizo na kinatarajiwa kujadili taarifa ya timu iliyoundwa kufanya tathmini ya kinachoendelea mashariki mwa DRC.

Katika kikao cha mawaziri wa mambo ya kigeni kilichofanyika juma lililopita mjini Harare, walipokea ripoti ya wakuu wa majeshi toka kwenye jumuiya hizo, ambapo wakatangaza kuunga mkono mpango wa mazungumzo kati ya waasi wa M23 na Serikali ya Kinshasa.

Waasi wa M23 wakiwa katika Mji wa Rubaya, 2025.
Waasi wa M23 wakiwa katika Mji wa Rubaya, 2025. © AFP – CAMILLE LAFFONT

Aidha katika kikao kilichopita cha wakuu wa nchi za SADC, walikubaliana kuwaondoa wanajeshi wao mashariki mwa DRC, hatua iliyokuja baada ya askari kadhaa kuuawa wakati waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda walipochukua mji wa Goma na Bukavu.

Wakuu hawa wan chi wanakutana wakati huu rais Felix Tshisekedi na mwenzake Paul Kagame, juma lililopita, walikutana ana kwa ana mjini Doha, Qatar na kukubaliana kwa pamoja kutafuta suluhu ya mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo.

Wakuu wa nchi za SADC na EAC wakati wa mkutano wa Dar es Salam, nchini Tanzania.
Wakuu wa nchi za SADC na EAC wakati wa mkutano wa Dar es Salam, nchini Tanzania. © Emmanuel Herman / REUTERS

Kikao cha hivi leo kitaongozwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa Kenya, William Ruto na mwenyekiti wa SADC rais wa Zimbabwe, Emerson Mnagangwa, ambapo watajadili ripoti ya mawaziri wa mambo ya nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *