Vikwazo; Fimbo ya Magharibi katika sera ya kigeni

Wakati Marekani na nchi za Ulaya zimekuwa na nafasi kubwa katika kuwawekea mashinikizo ya kiuchumi watu wa Syria kwa kutumia vikwazo vya kikatili, sasa baada ya kuanguka utawala wa Bashar al-Assad na kushika madaraka kundi la Hay’at Tahrir al-Sham, kuna minong’ono kwamba nchi hizo zina nia ya kupunguza vikwazo dhidi ya nchi hiyo.