Vikosi vya nchi kavu vya IRGC vyafanya maneva makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ya kujiandaa na vita

Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) vimeanza mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kushuhudiwa vya kujiweka tayari kwa vita katika eneo la kusini-magharibi mwa nchi, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuinua kiwango cha utayari wake wa kivita wa kukabiliana na vitisho vinavyoweza kutolewa na maadui.