Vifo vyapindukia zaidi ya 3,000 Myanmar baada ya tetemeko la ardhi

Zaidi ya watu 3,000 wamekufa nchini Myanmar katika tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa cha 7.7 kwenye kipimo cha Richter lililoikumba nchi hiyo siku sita zilizopita, kulingana na ripoti mpya utawala wa kijeshi iliyotoa siku ya Alhamisi, Aprili 3. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa utawala wa kijeshi amesema angalau watu 3,085 wamethibitishwa kufanriki na watu 545 walijeruhiwa.

Mapema wiki hii kiongozi wa kijeshi nchini Myanmar, Min Aung alisema kwamba kufuatia mkasa huo zaidi ya watu 4,500 wamejeruhiwa huku wengine takriban 440 hawajulikano walipo na matumaini ya kuwapata wakiwa hai ni hafifu.

Maeneo mengi ya nchi yaliyoathirika na tetemeko hilo yameachwa katika hali mbaya ikiwemo uharibifu wa miundombinu ikiwemo umeme, barabara na madaraja.

Huduma za kiutu zimeendelea kuzorota huku mashirika ya kimataifa yakiingilia kati kufanikisha huduma muhimu ikiwemo chakula, dawa na maji safi kwa waathirika wa tetemeko hilo.

Myanmar imekuwa katika hali ya machafuko tangu mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021, ambapo jeshi liliiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa kidemokrasia iliyoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi.

Machafuko hayo yamesababisha uasi wa silaha dhidi ya jeshi, na kuwalazimu zaidi ya watu milioni 3.5 kuyakimbia makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *