Vifo vya mafuriko vyafikia 205, Uhispania yakubwa na maafa mabaya zaidi katika historia ya sasa

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini Uhispania imeongezeka huku kukiwa na utabiri wa mvua nyingi zaidi, wakati nchi hiyo ikikumbwa na janga baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya sasa na baya zaidi kuwahi kutokea barani Ulaya katika miongo mitano.

Waokoaji wamesema idadi ya vifo vilivyosbabishwa na mafuriko hayo imepanda na kufikia 205, ambayo ni pamoja na 202 katika mkoa wa mashariki wa Valencia, wawili katika mkoa wa Castille-La Mancha kusini na mashariki mwa mji mkuu wa Madrid, na mmoja huko Andalusia kusini mwa Uhispania.

Maafisa wa serikali ya Uhispania wanasema idadi ya vifo huenda ikaongezeka huku matumaini ya kupata manusura yakififia na maiti zaidi za  makumi ya waliotoweka zikiendelea kupatikana.

Mvua kubwa iliyonyesha na mafuriko yaliyoanza Jumanne yamesababisha magari na madaraja kusombwa na maji, na miji kufunikwa na matope.

Uhispania

Timu za waokoaji, polisi na wazima moto wakiandamana na takriban wanajeshi 1,000 wanaendelea kutafuta manusura na wahanga wa mafuriko hayo.

Waziri wa Ulinzi wa Uhispania, Margarita Robles, alisema jana Ijumaa kwamba wanajeshi 500 zaidi wametumwa katika maeneo yaliyoathiriwa kusaidia juhudi za uokoaji.