
Takriban wahamiaji 190 waliofukuzwa kutoka Marekani walitua Venezuela Jumatatu jioni, Februari 10, wakiwa ndani ya ndege mbili zilizokodiwa na Caracas. Kurejeshwa nyumbani kwa wahamiaji hao kulikoelezewa na Rais Nicolas Maduro kama “hatua ya kwanza” kuelekea kurejesha uhusiano na Washington.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Raia wa Venezuela walitua kwenye uwanja wa ndege wa Maiquetia, kaskazini mwa Caracas, ndani ya ndege mbili za shirika la Conviasa siku ya Jumatatu, Februari 10, 2025. Baadhi walitoka wakiwa wameinua mikono yote miwili kusherehekea. Wengi walikuwa wamefungwa pingu ambazo zilitolewa kabla ya kupelekwa kwenye uwanja wa ndege, ambapo mamia ya polisi na wanajeshi walikuwa wakiwasubiri. “Tumechukua hatua nzuri, tena nzuri sana,” Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema kwenye televisheni, akisisitiza nia yake ya “kujenga” uhusiano wa “heshima, mawasiliano na maelewano” na Marekani.
Baada ya mjumbe wa Marekai kufanya ziara mwishoni mwa mwezi wa Januari , Caracas ilituma ndege hizi mbili, ikisisitiza matumaini yake ya “mwanzo mpya” kati ya nchi mbili ambazo hazijakuwa na uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 2019. Washington haimtambui Nicolas Maduro, mamlakani tangu 2013 na kuapishwa Januari kwa muhula wa tatu, kama rais halali wa nchi hiyo ya Amerika Kusini iliyo chini ya vikwazo vya Amerika Kusini.
Alipoapishwa mwezi Januari kwa muhula wa pili wa miaka minne, Donald Trump aliahidi kutekeleza kampeni kubwa zaidi ya kuwafukuza katika historia ya Marekani, akiahidi kuwarejesha mamilioni ya wahamiaji wasio na vibali, wengi wao kutoka Amerika Kusini.
Wakati wa kampeni yake, rais wa kihafidhina alishutumu mara kwa mara “uvamizi” wa wahamiaji, wanaoshutumiwa kwa “kutia sumu damu” ya Marekani na kusababisha wimbi la uhalifu – jambo ambalo hakuna takwimu rasmi zinazoonyesha.
“Wengi wa wahamiaji ni watu waaminifu”
Caracas ilisema abiria hao ni pamoja na washukiwa wa genge la Tren de Aragua, ambalo Donald Trump amelitangaza kuwa kundi la kigaidi. Serikali ya Venezuela, ambayo inadai kulisambaratisha ingawa viongozi wa genge hilo waliweza kutoroka na kundi hilo bado linaendelea, anaahidi kwamba wale wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi hilo”watachunguzwa vikali.” Hata hivyo, anabaini kwamba “kuna mazungumzo ya uwongo na yenye nia mbaya kuhusu suala la Tren de Aragua (…) kuwaadhibu wahamiaji wote wa Venezuela na kuinyanyapaa nchi yetu (…). Wengi wa wahamiaji ni watu waaminifu na wachapa kazi.
Venezuela imepanga mara kwa mara safari za ndege za kuwarejesha wahamiaji kutoka Marekani na nchi nyingine za Amerika Kusini kama sehemu ya mpango wake wa “Kurudi Nchini”, mara nyingi husherehekewa kwa propaganda nyingi.