
Tathmini ya jinai za utawala wa Kizayuni katika miaka ya hivi karibuni, inatoa uwezekano wa kuwepo uratibu wa hatua ya kichokozi ya hivi karibuni ya utawala huo dhidi ya Iran na shambulio la kigaidi lililotekelezwa na magaidi wa Jeish Dhulm katika eneo la kusini mashariki mwa nchi.
Jumamosi alfajiri, utawala wa Kizayuni ulishambulia vituo vya kijeshi katika mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam ambapo mfumo jumuishi wa ulinzi wa anga wa Iran ulifanikiwa pakubwa kukabiliana na hatua hiyo ya kichokozi.
Sambamba na uchokozi huo wa Israel, Kituo cha Habari cha Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kilitangaza siku hiyo hiyo ya Jumamosi asubuhi kuuawa shahidi kwa wafanyakazi kumi wa vitengo viwili vya doria vya kituo cha polisi cha Gouharkuoh katika mji wa Taftan. Katika mapigano yaliyotokea, idadi ya maafisa wa polisi na askari wa kituo cha polisi cha Gouharkouh katika mji wa Taftan waliuawa shahidi.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kila mara utawala wa Kizayuni unapofeli kufikia malengo yake ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huamua kufidia kushindwa huko kwa kulitumia kundi la kigaidi linalojiita Jaish al-Adl, ambalo linashirikiana na makundi mengine ya kigaidi yanayopinga Mapinduzi ya Kiislamu kutekeleza vitendo vya kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia kusini mashariki mwa nchi.
Kundi hilo la kigaidi ambalo limekuwa likifanya oparesheni za kipofu dhidi ya watu wasio na ulinzi limekuwa likitumiwa na utawala ghasibu wa Israel kutekeleza mashambulio ya kigaidi mara kwa mara dhidi ya maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutumia visingizio mbalimbali.