Manchester, England. Manchester United imepanga kujenga Uwanja mpya ambao utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 100,000 tofauti na wa sasa unaobeba mashabiki 74,310.

Muonekano wa nje ya uwanja mpya wa Manchester United ukionyesha njia iliyopewa jina la Wembley iliyopambwa na miti kuelekea uwanjani. Picha na mtandao
Uwanja huo wa kisasa utakuwa na minara mitatu mikubwa kama ilivyo kwenye nembo ya timu hiyo. Minara hiyo itabeba mwamvuli mkubwa wa kioo ambao utafunika sehemu ya Uwanja kuhakikisha mashabiki wanakaa kwenye mazingira yasiyoathiriwa na mvua.

Muonekano wa uwanja mpya wa Manchester United utakavyokuwa wakati wa usiku. Picha na mtandao
Uwanja huo mpya utajengwa pembeni kidogo na ulipo uwanja wa sasa wa Old Trafford ambao umetumika kwa miaka 115, United imepanga kugharamia ujenzi wa uwanja huo kwa Dola 2. 996 bilioni (Sh6 trilioni).

Muonekano wa uwanja mpya wa Manchester United wenye muundo wa kisasa. Picha na mtandao