Uungaji mkono wa Marekani kwa hatua ya utawala wa Kizayuni dhidi ya UNRWA

Rais Donald Trump wa Marekani ameendeleza uungaji mkono wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kufuta idhini ya serikali ya Biden kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), na kutangaza kuwa anaunga mkono uamuzi wa utawala huo wa kufunga ofisi ya UNRWA huko Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu.