Uturuki: Rais Erdogan ataka kugawanya upinzani

Nchini, uchunguzi na watu kukamatwa vimeongezeka katika wiki za hivi karibuni katika safu ya upinzani dhidi ya Rais wa Uturuki Erdogan. Wanalenga zaidi CHP, chama kikuu cha upinzani. Huko Istanbul, viongozi zaidi ya kumi waliochaguliwana maafisa wa manispaa kutoka chama hiki waliwekwa chini ya ulinzi sik ya Jumanne asubuhi, Februari 11, kwa madai ya kuhusishwa na “ugaidi.”

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Ankara, Anne Andlauer

Chama cha Republican People’s Party (CHP) kilishinda uchaguzi wa mameya katika wilaya 26 kati ya 39 za Istanbul mnamo mwaka 2023. Katika miezi ya hivi karibuni, mameya wake wawili wamefungwa.

Watu kukamatwa siku ya Jumanne, Februari 11, kunawahusu manaibu meya na madiwani wa manispaa kutoka wilaya nyingine saba, wote wakituhumiwa kuhusishwa na ugaidi. Katika kesi hii, na PKK, Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan wanahusishwa na ugaidi.

Kugawanya upinzani

Hata hivyo wakati huo huo, serikali ya Uturuki inafanya mazungumzo na kiongozi anayefungwa wa PKK, Abdullah Öcalan, ambaye anatarajiwa hivi karibuni kutoa wito kwa vuguvugu lake kuachana na silaha. Chama kinachounga mkono Wakurdi, DEM, kinahusika moja kwa moja katika juhudi hizi za amani.

Mtaalamu wamasuala ya siasa Seren Selvin Korkmaz, anasema hii sio kitendawili: “Serikali, kwa upande mmoja, inafanya ufunguzi kwa Wakurdi. Kwa upande mwingine, inaweka shinikizo kwa wahusika wengine wa upinzani, haswa CHP. Na kwa sababu inamuweka chini ya shinikizo, inamzuia kuunga mkono waziwazi juhudi za amani, jambo ambalo linaweza kuwa na athari ya kuleta mpasuko kati ya wahusika wa vuguvugu la kisiasa la Wakurdi na wapinzani wengine. Kati ya DEM na CHP. Serikali inajaribu kuvunja muungano wa upinzani. “

Ni muungano huu wa kimya kimya wa vyama vya upinzani na wapiga kura wao ambao ulimlazimu Recep Tayyip Erdogan kukabili duru ya pili katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2023 kwa mara ya kwanza na kushindwa katika uchaguzi wa manispaa wa mwaka jana.