
Kukamatwa na kufungwa kwa Meya wa Istanbul Ekrem Imamoğlu kumeendelea kuhamasisha umati wa watu tangu Machi 19. Wafuasi kadhaa wa upin,zani wamekamatwa na vikosi vya usalama kulingana na vyanzo kadhaa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Katika siku ya sita ya maandamano hayo, ambayo kwa kiasi kikubwa yameshika kasi kutokana na makundi ya wanafunzi, mwenyekiti mkuu wa Chama cha Republican People’s Party (CHP), Özgür Özel ametoa wito Jumatatu Machi 24 wa kususia vifaa vinavyotengenezwa na makampuni yanayounga mkono serikali yanayomilikiwa na vigogo ambao pia wanamiliki vyombo vikuu vya habari ambavyo vimepiga marufuku kurushwa kwa picha za maandamano ya hivi majuzi.
“Erdoğan ajiuzulu!” “, ni kauli mbiu inayorudiwa tena na tena na makumi ya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika wilaya ya Fatih, katika uwanja wa manispaa kuu ya Istanbul, anaripoti mwandishi wetu huko Istanbul, Céline Pierre-Magnani.
Özgür Özel, mwenyekiti wa chama cha Ekrem Imamoğlu, amlijitokea jukwaani na kuhutubia umamatu wa waandamanaji. Mkutano wa kila siku na umati wa watu, ambao umekuwa wa kitamaduni tangu kukamatwa kwa meya wa Istanbul mnamo Machi 19, ambaye ameteuliwa kuwa mgombea wa CHP katika uchaguzi wa rais wa 2028.
“Huu sio mkutano wa hadhara, lakini ni kitendo cha dharau dhidi ya ufashisti,” Özgür Özelme makumi ya maelfu ya watu waliokusanyika mbele ya manispaa ya Istanbul. “Wazikeni wanaowapuuza,” amesema pia, akirejelea vituo vya televiheni na redio zinazounga mkono serikali ambazo hazirushi hewani picha za maandamano hayo.
Mamlaka nchini Uturuki imesema, inawashikilia zaidi ya watu 1,100 kufuatia maandamano makubwa yaliyozuka wiki iliyopita baada ya kukamatwa meya wa mji wa Istanbul na mpinzani mkuu wa rais wa nchi hiyo Recep Tayip Erdogan, Ekram Imamglo.
Maandamano hayo ya maelfu ya watu yalianza mjini Istanbul baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani na kuenea katika zaidi ya majimbo 55 kati ya 81 ya Uturuki, na kusababisha makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia na kulaaniwa kimataifa.
Mbali na kukamatwa kwa watu hao, Uturuki imekuwa ikizifungia akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii za watu wanaohamaisha maandamnao nchini humo.Mahakama ya Uturuki yaamuru kuzuiliwa kwa Meya wa Istanbul
Hali kadhalika, Ekram Imamglo anayetuhumiwa kwa ufisadi na ugaidi anatajwa kuwa mwanasiasa pekee ambaye anaweza kumshinda rais wa Uturuki Erdogan katika uchaguzi mkuu ujao na tayari chama chake cha CHP kimempitisha kwa mgombea mkuu katika uchaguzi wa 2028.