Utawala wa Trump kutuma karibu wanajeshi 3,000 wa ziada mpakani na Mexico

Jeshi la Marekani limetangaza siku ya Jumamosi kutumwa kwa karibu wanajeshi 3,000 wa ziada kwenye mpaka na Mexico, na kufikisha karibu 9,000 idadi ya wanajeshi waliokusanywa kwenye eneo hili kwa ajili ya mapambano dhidi ya wahamiaji haramu, ambayo yalipewa kipaumbele na utawala wa Trump.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hawa watasaidia vikosi vya polisi vya mpakani “kudumisha usalama kwenye mpaka wa kusini,” kamandi ya jeshi la Marekani kwa Amerika Kaskazini (Northcom) imesema katika taarifa.

Jeshi “halitaongoza wala kuhusika katika kuzuia (wahamiaji) wala katika shughuli za kuwafukuza”, lakini watawajibika kwa ujumbe wa ufuatiliaji, usaidizi wa utawala na usaidizi wa vifaa, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uwezo wa usafiri wa anga, taarifa hiyo ilibainisha.

“Kutumwa huku kwa wanajeshi hawa kutatoa wepesi zaidi na usaidizi wa kushughulikia wimbi lwahamiaji haramu na dawa za kulevya katika mpaka wa kusini,” kamanda wa Northcom Jenerali Gregory Guillot amesema katika taarifa hiyo.

Katika siku yake ya kwanza kurejea White House, Donald Trump alitia saini agizo la utendaji kutangaza hali ya hatari kwenye mpaka na Mexico.

Siku mbili baadaye, aliamuru kutumwa kwa askari 1,500 wa ziada. Anaishutumu Mexico kwa kutofanya vya kutosha dhidi ya uhamiaji haramu na uingizaji nchini Marekani wa fentanyl, dawa yenye nguvu ambayo inaleta uharibifu nchini humo.

“Uvamizi”

Wakati wa kampeni za uchaguzi, chama cha Republican kiliwashutumu wahamiaji kuwa “wahalifu” ambao “wanatia sumu damu” ya Marekani na kuahidi kutekeleza “operesheni kubwa zaidi ya kuwafukuza katika historia ya nchi.”

Baadhi ya wahamiaji milioni 11 wasio na vibali walikuwa wakiishi Marekani mwaka 2022, kulingana na makadirio ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Usalama wa Nchi.

Kikosi cha Doria cha Mpakani cha Marekani kimesema kilikamata takriban milioni 8.8 ya wahamiaji haramu katika mpaka na Mexico, mara kadhaa, katika kipindi cha miaka minne ya muhula wa Rais wa zamani kutoka chama cha Democratic Joe Biden. Kukamatwa huku kulishika kasi mwishoni mwa mwaka 2023 kabla ya kupungua sana mwishoni mwa muhula wake.

Ili kuharakisha kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali, serikali yake inaweka shinikizo kwa nchi za Amerika Kusini kukubali kurejea kwa raia wao.

Nchini Marekani, rais kutoka chama cha Republican ameanza kushambulia majimbo na miji vinavyoitwa “mahali patakatifu” ambavyo vinakataa kushirikiana na sera ya mamlaka ya shirikisho ya kuwafukuza wahamiaji haramu.

Serikali yake pia inapanga kuwazuilia hadi wahamiaji haramu 30,000 katika kambi ya jeshi la Marekani huko Guantanamo nchini Cuba, na kuongeza takribani maeneo 40,000 ambayo tayari yapo katika kambi za kizuizini kote Marekani.