
Utabiri wa kampuni ya takwimu za soka ya Opta, umeipa Liverpool nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Arne Slot, imepewa asilimia 17.2 ya kuondoka na taji la mashindano hayo msimu na ndio timu iliyopata asilimia nyingi.
Timu inayopewa nafasi ya pili ni Barcelona ambayo Opta imeipatia asilimia 15.4 za kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu.
Katika hatua ya 16 bora, Barcelona imepangwa kukutana na Benfica na iwapo itasonga mbele, katika robo fainali itacheza na mshindi wa mchezo baina ya Borussia Dortmund na Lille.
Timu ambayo inashika nafasi ya tatu kwa asilimia za kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kwa mujibu wa utabiri wa Opta ni Arsenał.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Mikel Arteta, katika hatua inayofuata imeangukia kwa PSV na iwapo itafanikiwa kusonga mbele, itakabiliana na mshindi baina ya Real Madrid na Atletico Madrid.
Nafasi ya nne katika utabiri huo imeangukia kwa miamba ya Ligi Kuu ya Italia, Inter Milan ambayo yenyewe imepewa asilimia 12.7.
Katika hali ya kushangaza mabingwa watetezi na wa kihistoria wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid wamewekwa katika nafasi ya tano kwenye utabiri huo wakipa