Usiku wa Grammy ulivyoweka rekodi kwa mastaa

Marekani. Kati ya vitu ambavyo Beyonce hatakuja kuvisahau ni tukio la Grammy 2025, lililofanyika Februari 2, 2025  katika ukumbi wa Crypto.com huko Los Angeles baada ya kuinyakua tuzo ya Albamu Bora aliyokuwa akiisotea kwa miaka mingi.

Beyonce ambaye anashikilia rekodi ya msanii anayeongoza kuwania tuzo hizo kwa mara 99 pia ndiye msanii anayeshikilia rekodi ya msanii aliyechukua tuzo za Grammy mara nyingi zaidi akibeba mara 34 ndani ya miaka tofauti tofauti, ameibuka kidedea katika vipengele viwili cha Albamu Bora ya Mwaka ‘Cowboy Carter’ na Country Group Perfomance.

                           

“Ningependa kuwashukuru familia yangu nzuri. Wote wasanii walioshirikiana nami. Asanteni. Albamu hii isingekuwa hivi bila ninyi. Ningependa kumshukuru Mungu tena, na mashabiki wangu. Bado nipo kwenye mshtuko, hivyo asanteni sana kwa heshima hii,” amesema Beyonce wakati akichukua tuzo yake.

                     

Hata hivyo, katika tuzo hizo za 67 za Grammy zilizoanza kufanyika tangu Mei 4, 1959. Mwanamuziki wa Hip-hop Kendrick Lamar ameshinda vipengele vitatu kati ya vipengele saba alivyokuwa akiwania ambavyo ni ‘Best Rap Song’, ‘Best Rap Perfomance’na ‘Best Msic Video’. Huku akiwa anatimiza jumla ya tuzo 20 za Grammy kwenye kabati lake la tuzo.

Naye Chris Brown, katika usiku huo alifanikiwa kuweka rekodi mpya katika tasnia ya muziki baada ya kushinda tuzo yake ya pili. 

Vipengele alivyoshinda ni Best R&B Albamu kupitia albamu yake mpya 11:11 (Deluxe), ikiwa ni ushindi wake wa pili tangu aliposhinda tuzo yake ya kwanza mwaka 2012 kwa albamu F.A.M.E. 

Mbali na ushindi huu, Brown aliteuliwa katika vipengele vitatu kwenye tuzo hizo, vikiwemo Best R&B Performance kwa wimbo wake Residuals na Best African Music Performance kwa kolabo yake Sensational. 

                       

Aidha mwanamuziki wa Nigeria Tems, ameibuka mshindi wa Grammy 2025 katika kipengele cha Best African Music Perfomance.

Ushindi huo ambao ameupata kupitia wimbo wake ‘Love Me Jeje’, unaenda kuwa wa pili baada ya mwaka jana kushinda katika kipengele cha Best Melodic Rap Perfomance ‘Wait For You’. 

Utakumbuka katika kipengele cha Best African Music Performance ambacho ameshinda Tems alikuwa akishindana na wasanii wengine kama Davido, Burna Boy ‘Higher’, Chris Brown & Lojay ‘Sensational’, Yemi Alade ‘Tomorrow’, pamoja na Asake & Wizkid MMS.

Baadhi ya washindi Grammy 2025…

Album of the Year

Mshindi: Beyoncé – Cowboy Carter

Record of the Year

Mshindi: Kendrick Lamar – Not Like Us

Song of the Year

Mshindi: Kendrick Lamar – Not Like Us

Best new artist

Mshindi: Chappell Roan

Best Pop duo/group performance

Mshindi: Lady Gaga & Bruno Mars – Die With A Smile