Ushuru wa Marekani: Jinsi Afrika Kusini inataka kupunguza madhara yake

Masoko yameshuka Aprili 7, 2024, kutokana na uamuzi wa rais wa Marekani juu ya ushuru aliotangaza dhidi ya ulimwengu. Donald Trump anawashutumu washirika wa kiuchumi wa Marekani kwa “kuwapora”. Wakati baadhi wakiahidi jibu, wengine wanajaribu kujipanga ili kupunguza madhara, kama vile Afrika Kusini, ambayo imeathirika zaidi. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu maalum mjini Pretoria, Valentin Hugues

Uchumi wa kimataifa bado uko katika msukosuko kufuatia uamuzi wa Marekani wa kutoza ushuru mkubwa wa forodha kwa takriban washirika wake wote wa kibiashara. Wakati baadhi yao wanaahidi kulipiza kisasi (China, EU, Canada), wengine, kama vile Zimbabwe, wamechagua kutotoza ushuru wa bidhaa zote za Marekani kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wake, Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa zaidi na ushuru wa forodha wa Marekani, kwa 31% ya ushuru kwa bidhaa za Afrika Kusini na 25% kwa sekta ya magari.

Mnamo tarehe 4 Aprili, Wizara za Uhusiano wa Kimataifa na Biashara zilifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ili kuzungumza kwa sauti moja na kutafuta suluhisho: yaani, kujadili mikataba na Marekani, lakini pia kuimarisha uhusiano wa kibiashara na washirika kama vile Ulaya, au kufungua masoko mapya, hasa katika Asia.

“Tunawaambia Wamarekani kwa kujadili maslahi yao wenyewe” 

Kodi hizi mpya za Marekani zinafuta kikamilifu mapendeleo ya ushuru ya AGOA (African Growth and Opportunity Act au “Sheria kuhusu Ukuaji na Fursa Afrika”) kwa sekta nyingi. Mkataba huu, ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 20, uliwezesha, kwa mfano, usafirishaji wa magari na bidhaa za chakula bila ushuru wa forodha.

Kwa muda mfupi, Afrika Kusini kwa hiyo inataka kushawishi Marekani kufanya upya AGOA.

Parks Tau, Waziri wa Biashara na Viwanda, amebainisha: “Marekani imethibitisha kwamba mkutano wa kilele wa AGOA utafanyika mwaka huu. Tutalazimika kujadiliana kwa kuzingatia mbinu ya Marekani, ambayo haitaki tena makubaliano ambayo yanapendelea upande mmoja tu. Kwa kuwa tuna hakika kwamba AGOA pia ina maslahi kwao, changamoto itakuwa kuonyesha hili kwao. Kwa kweli tunahitaji kuwaambia Wamarekani kwa kujadili masilahi yao wenyewe. ” 

Lakini maamuzi ya hivi majuzi ya Ikulu ya Marekani yanaonekana kuashiria mwisho wa makubaliano haya ya kibiashara. Kwa hivyo nchi lazima ijiandae kwa siku zijazo na kufikiria kwa muda mrefu. Kwa kuiangalia China, kwa mfano, anafafanua naibu mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Xolelwa Mlumbi-Peter: “Tunaangalia masoko mapya katika Mashariki ya Kati na Asia, ambapo bado hatuna fursa ya kupata fursa nzuri. Tayari kuna majadiliano yanaendelea na wazalishaji wa China ili kujiimarisha hapa.” 

Afrika Kusini pia inataka kutumia urais wake wa G20 mwaka huu kuzingatia msimamo mpya wa kodi ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *