
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa “mkataba mkubwa wa kibiashara” utatangazwa leo Alhamisi asubuhi mjini Washington, ikiwa ni mara ya kwanza tangu utawala wake uweke msururu wa ushuru kwa bidhaa za kigeni.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Mkutano mkubwa na waandishi wa habari kesho asubuhi saa 4 (sawa na saa 10alasiri sa za Ufaransa) katika Ofisi ya Oval kuhusu mpango mkubwa wa biashara na wawakilishi wa nchi kubwa na inayoheshimika sana,” raid Trump ameandika kwenye mtandao wake wa Truth Social.
Msururu wa kwanza kati ya mfululizo mrefu, uameongeza Donald Trump, kwa herufi kubwa kama kawaida, bila kutoa maelezo zaidi juu ya upeo wa makubaliano au nchi husika.
Kulingana na Gazeti la New York Times, inaweza kuwa Uingereza. Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Donald Trump waliripoti “mazungumzo yenye tija” mwishoni mwa mwezi Machi.
Tangu arejee madarakani, rais huyo wa Marekani amesababisha tetemeko la ardhi la kiuchumi, hasa kwa kile alichokiita Siku ya Ukombozi mnamo Aprili 2, alipoweka ukuta wa ushuru mpya kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani.
Tangu wakati huo, Donald Trump amebadili mkondo wake kwa muda wa siku 90, na kuahidi makubaliano na washirika wakuu wa Marekani kupunguza mswada huo. Kufikia hatua hii hakuna kilichotangazwa.
Lakini majadiliano yanaendelea na nchi kadhaa kama vile Canada, Korea Kusini na Vietnam.
Maafisa wa Marekani na China pia wanakutana nchini Uswisi mwishoni mwa juma kuweka msingi wa mazungumzo. China ndio mlengwa mkuu wa Donald Trump, ambaye ameweka ushuru wa 145% kwa bidhaa “zilizotengenezwa China.”
Beijing ililipiza kisasi kwa kutoza ushuru wake wa 125% kwa bidhaa za Marekani.