Ushuru wa chuma na aluminium: EU yalipiza kisasi na kulenga bidhaa ‘zilizotengenezwa Marekani’

Tume ya Ulaya imetangaza leo Jumatano asubuhi, Machi 12, kwamba itatoza ushuru wa forodha “wenye nguvu lakini wenye uwiano” kwa msururu wa bidhaa za Marekani kuanzia Aprili 1, 2025, kujibu ushuru wa 25% wa Marekani kwa chuma na aluminium.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Majibu ya Ulaya kwa ushuru wa 25% wa Marekani kwa chuma na aluminiu utafanyika katika hatua mbili. Kuanzia Aprili 1, 2025, hatua za kukabiliana na Umoja wa Ulaya zilizowekwa mwaka wa 2018 na 2020 kutokana na ushuru wa forodha za Marekani wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump zitarejeshwa kiotomatiki, na kusimamishwa kwao kumalizika tarehe 31 Machi. “Kwa mara ya kwanza, hatua hizi za kusawazisha zitatekelezwa kwa ukamilifu. “Ushuru wa forodha utatumika kwa bidhaa kuanzia boti hadi vinywaji kupitia pikipiki,” Tume ya Ulaya imeeleza.

Masikitiko

Umoja wa Ulaya “unasikitika sana” hatua zilizoamuliwa na Rais Donald Trump, Rais wa Tume Ursula von der Leyen amesema katika taarifa. “Ushuru wa forodha ni kodi. Ni mbaya kwa biashara na mbaya zaidi kwa watumiaji,” ameongeza. “Ajira ziko hatarini. Bei zitapanda, Ulaya na Marekani.

Tume ya Ulaya inakadiria kuwa hatua za Marekani zitaathiri bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 28, au euro bilioni 26. Imetangaza kuwa majibu ya EU yangeathiri kiasi sawa cha bidhaa za Marekani. Ushuru wa 25% kwa chuma na aluminium unaotafutwa na Rais Donald Trump umeanza  kutekelezwa siku ya Jumatano, Machi 12 saa sita na dakika moja (00:01) usiku, kuashiria hatua mpya katika vita vya kibiashara kati ya Marekani na washirika wake wakuu.

“Majibu yenye ufanisi”

Canada, China, Umoja wa Ulaya, Japani na Australia zote zimeathirika, huku lengo la Bw. Trump likiwa ni kulinda sekta ya chuma ya Marekani, ambayo imeshuhudia uzalishaji wake ukishuka mwaka baada ya mwaka, kutokana na ushindani mkubwa, hasa kutoka Asia. Rais wa Marekani alikuwa tayari ametoza ushuru wa uagizaji wa chuma na aluminium katika muhula wake wa kwanza (2017-2021), lakini ushuru huu mpya unakusudiwa kuwa “bila ubaguzi na bila kusamehewa,” amehakikisha ilipotangazwa mapema mwezi wa Februari.

Hatua ya kwanza ya utaratibu wa Ulaya ni “awamu ya mashauriano ya wiki mbili na wadau wa EU” ili kuhakikisha kuwa “bidhaa zinazofaa” zinalengwa na “kuhakikisha jibu la ufanisi (…) kupunguza usumbufu kwa biashara na watumiaji wa Ulaya.” Hatua hizi za ziada zinapaswa kuanza kutumika katikati ya Aprili.

Ushuru huu wa forodha wa Marekani “haufai kabisa,” Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese pia alijibu mnamo Machi 12. “Hii sio ishara ya kirafiki,” waziri mkuu wa Australia aliwaambia waandishi wa habari baada ya kushindwa kujadili msamaha wa dakika ya mwisho. Msisimko wa matangazo ya Marekani kuhusu ushuru mpya wa bidhaa unazidi kuongezeka sokoni: Wall Street imefuta karibu mafanikio yote yaliyopatikana tangu kuchaguliwa kwa Donald Trump katika siku za hivi karibuni, huku kukiwa na hofu ya kuzorota kwa uchumi nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *