
China imeapa siku ya Ijumaa kuchukua “hatua zote muhimu” baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa ataweka ushuru wa ziada wa 10% kwa bidhaa za China zinazoagizwa kutoka nje.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Ikiwa Marekani itaendelea kufuata njia hii, China itachukua hatua zote muhimu ili kutetea haki na maslahi yake halali,” Wizara ya Biashara imesema katika taarifa iliyoripotiwa na shirika la hbari la AFP.
Hatua hii mpya kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump itaanza kutumika siku ya Jumanne Machi 4, 2025. Inachochea hofu ya vita vipya vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani. Ushuru huu mpya wa 10% kwa bidhaa kutoka China utaongezwa kwa ushuru wa kiwango sawa, ambacho tayari kimewekwa na Donald Trump mwanzoni mwa mwezi wa Februari dhidi ya bidhaa kutoka China. Rais wa Marekani anaishutumu Beijing kwa ulanguzi wa fentanyl, dawa ambayo inaharibu maisha ya watu wengi katika ardhi ya Marekani.
“Kukimbia majukumu”
“Hii ni kawaida ya kile kinachoitwa kulaumu wengine na kukwepa jukumu,” msemaji wa Wizara ya Biashara ya China amesema katika taarifa yake leo Ijumaa. “China ni moja ya nchi zilizo na sera kali na za kina zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani” na imekuwa ikishirikiana kikamilifu “na Marekani na nchi nyingine duniani kote” katika suala hili, amebainisha “Lakini Marekani imechagua kupuuza ukweli huu tangu mwanzo,” msemaji huyo aamesema. “Ikiwa Marekani itaendelea na nji hii, China haitasita kutetea haki zake zote,” ameongeza katika taarifa.
Taarifa hiyo pia inabaini kwamba ushuru mpya wa forodha “utaongeza mzigo kwa makampuni na wanunuzi wa Marekani na kuathiri uthabiti wa mlolongo wa kimataifa wa viwanda.”