Ushindi wampa jeuri Kaseja

USHINDI mtamu buana. Baada ya kuiongoza Kagera Sugar katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho na zote kuibuka na ushindi, kocha mkuu wa Kagera, Juma Kaseka ametamba kwamba ameanza kuona mwanga na morali imeongezeka zaidi kwa wachezaji wa timu hiyo.

Kaseja alikabidhiwa mikoba iliyoachwa wazi na Melis Medo aliyetimkia Singida Black Stars baada ya timu hiyo kuwa na matokeo mabaya, lakini kipa huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania alianza na ushindi wa 2-1 dhidi ya Pamba Jiji katika Ligi Kuu kabla ya juzi kuizima Namungo kwa mabao 3-0 zilipokutana katika hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho (FA).

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja aliyerejesha katika timu hiyo baada ya awali kuwa kocha wa makipa na kuondoka, alisema ushindi iliyopata Kagera unazidi kuongeza morali kwa wachezaji katika kupambana wakiamini bado kuna nafasi ya wao kufanya vizuri kwa michezo iliyopo mbele yao.

“Nawapongeza wachezaji kwa kupambana na kunipa nguvu ya kuongeza mbinu zaidi kwenye uwanja wa mazoezi ili niweze kuipambania Kagera ifike fainali ya FA, pia kubaki Ligi Kuu msimu ujao,” alisema Kaseja na kuongeza;

“Sio kazi rahisi, lakini mipango mizuri na kupambana kwa wachezaji hakuna kinachoshindikana, tuna timu nzuri makosa machache ndio yanatugharimu nina imani kubwa na kikosi nilichonacho naamini tutafanya kitu kikubwa.”

ZILIZOBAKI KAGERA

v Coastal Union,

v Prisons, 

 v Dodoma Jiji,

 v Azam FC,

v Namungo, v Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *