Ushindi wa Tems Grammy, Davido ataacha muziki?

Marekani. Mwanamuziki wa Nigeria Tems ameibuka mshindi wa Grammy 2025 katika kipengele cha Best African Music Perfomance.

Ushindi huo ambao ameupata usiku wa kuamkia leo Februari 3, 2025 kupitia wimbo wa Love Me Jeje, unaenda kuwa wa pili baada ya mwaka jana kushinda katika kipengele cha Best Melodic Rap Perfomance ‘Wait For You’. 

                    

Hata hivyo, ushindi wa Tems unaenda  kuzalisha deni kwa Davido kwani jana Februari 2,2024 aliahidi kuwa endapo asipoondoka na Grammy 2025 ataacha kufanya muziki.

“Kama sitoshinda Grammy mwaka huu ninafikiria kuacha muziki, nimeweka moyo wangu na roho yangu kwenye kazi, najituma kuliko msanii yeyote ndani ya Afrika.  Daima mimi ndiye huwa mbele naiongoza Afrobeat, naongoza mashambulizi, naitengeneza aina hii ya muziki. 

                     

“Mimi ndiyo jina kubwa kwenye Afrobeat, hilo halina mashaka, lakini kabati langu la tuzo haliakisi machozi, jasho na damu nilivyowekeza. Kuchaguliwa kugombea Grammy kwa miaka 2 mfululizo kumenipa furaha, lakini pia hii ni dawa chungu kuimeza. Kama Grammy wangekua kweli wana usawa, ningeshachukua takribani tunzo 20 hadi hivi sasa,”amesema Davido.

                         

Utakumbuka Davido ametoka patupu kwenye kipengele cha Best African Music Performance ambacho ameshinda Tems

Wasanii wengine waliochuwana na Tems ni Burna Boy  ‘Higher’, Chris Brown & Lojay ‘Sensational’, Yemialade ‘Tomorrow’, pamoja na Asake & Wizkid MMS.