Urusi yarusha makombora Odesa na Kyiv nchini Ukraine

Urusi yarusha makombora Odesa na Kyiv nchini Ukraine

Baada ya Urusi kuvurumisha droni zaidi ya 300 na makombora saba nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky amewatolea mwito washirika wake ambao ni mataifa ya Magharibi kujibu kwa kuichukulia hatua kali Urusi. 

Zelensky aliandika katika mitandao yake ya kijamii kwamba angelipenda Marekani ichukue hatua huku akisema taifa hilo lina nguvu ya kuilazimisha Urusi kuingia katika makubaliano ya amani. Aliendelea kuandika kuwa Ulaya ambayo haina budi ila kuungana kwa nguvu moja pia inapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya Urusi kufuatia hatua yake hiyo ya kuendelea kulishambulia taifa lake. 

Mtu mmoja auwawa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine

Wakati huo huo, Gavana wa Odesa, Oleg Kiper, amesema watu wawili wameuwawa katika mashambulizi hayo ya Urusi yaliyofanywa usiku wa kuamkia leo katika makaazi ya watu mjini humo. Watu wengine tisa walijeruhiwa katika mkasa huo. Urusi pia inadaiwa kulenga hospitali inayotoa huduma za kujifungua, eneo la dharura na makaazi ya watu. Gavana Kiper amesema watu wote waliokuwa katika hospitali hiyo ya wanawake waliondolewa kabla ya eneo hilo kulengwa. 

Urusi imezidisha mashambulizi yake Ukraine ambayo pia imekuwa ikijibu mashambulizi ya Moscow kwa kushambulia maeneo ya ndani ya Urusi wakati mazungumzo yaliyofanyika mjini Istanbul, Uturuki, yakifeli kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa miaka mitatu. 

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wa kijeshi huku mapigano yakiendelea 

Ukraine 2025
Urusi na Ukraine zakubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa wa kijeshi.Picha: Ukraine’s President Volodymyr Zelenskiy via Telegram/REUTERS

Kando na makubaliano ya kubadilishana wafungwa, hakuna tena hatua zilizipigwa kuelekea amani ya kudumu ya mataifa hayo mawili huku Urusi ikikataa miito ya kutokuwa na masharti kuelekea makubaliano hayo ya usitishwaji wa vita. 

Mataifa hayo mawili jirani na hasimu yalibadilishana wafungwa wa kijeshi. Muda mfupi baada ya hatua hiyo, Rais Zelensky alisema mabadilishano hayo yataendelea hatua kwa hatua ndani ya wiki kadhaa zijazo. Mpango huo utajumuisha kuwaachia wanajeshi wote wanaoshikiliwa walio kati ya miaka 18 hadi 25, wanajeshi wagonjwa pamoja na miili ya wanajeshi waliouwawa wakati wa vita. 

Ukraine yaishambulia Urusi na kuulenga mji mkuu Moscow na miundombinu muhimu

Hata hivyo, kando na hatua hiyo Zelensky alisema wazi kwamba haina maana kuendelea na mazungumzo na ujumbe wa Urusi kutokana na ujumbe huo kukataa kufikia makubaliano ya kusitisha vita. Mkuu wa Ujumbe wa Ukraine, Andriy Yermak, alisema ni muda wa kila mtu kutambua kuwa Urusi inaelewa lugha tu ya mapigano na sio mazungumzo. 

Moja ya masharti ya Urusi kukubali mpango wa kusitisha mapigano ni Ukraine kuridhia kuyaachia maeneo yake yaliyotekwa na Urusi na kutojiunga na Jumuiya ya kujihami NATO. 

Urusi imekataa kusitisha mapigano kwa siku 30 ikisema hatua hiyo izaipa Ukraine nafasi ya kujipanga upya. Ukraine nayo inataka Urusi iondoke kikamilifu katika maeneo yake iliyoyanyakua na pia hakikisho la usalama kutoka Magharibi. 
 

SIku 1,000 za vita vya Ukraine

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *