Urusi yaendeleza mashambulizi makali ya droni Ukraine

Maafisa wa Ukraine wamesema kulikuwa na milipuko kadhaa katikati ya Kyiv pamoja na milio ya makombora, huku mifumo ya ulinzi ikijaribu kuzidungua baadhi ya droni. Majengo na magari katika maeneo kadhaa ya mji huo yaliwaka moto.

Katika mji wa kusini wa bandari wa Odesa, mtu mmoja aliuawa na wengine wanne wakajeruhiwa katika shambulizi la droni. Meya wa mji huo amesema makombora ya Urusi yalivipiga vituo vya kina mama wajawazito na hospitali ambazo tayari watu walikuwa wamehamishwa.

Wakati huo huo, Urusi na Ukraine zilibadilishana mamia ya wafungwa wa kivita na raia hapo jana. Waliorudishwa makwao ni pamoja na askari waliojeruhiwa, na wale walio chini ya umri wa miaka 25. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mchakato huo ni mgumu sana, na kwamba kuna maelezo mengi nyeti, na mazungumzo yanayoendelea karibu kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *