Urusi yadai kuingia mkoa wa Ukraine wa Dnipropetrovsk

Wizara hiyo ya Urusi ilisema askari wa ardhini walifika kwenye mpaka wa magharibi wa mkoa wa Donetsk na wanaendelea na mashambulizi yao kwenye eneo la Dnipropetrovsk. Madai hayo pia yaliungwa mkono na naibu mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi la Urusi Dmitry Medvedev. Lakini mkuu wa majeshi ya Ukraine mjini Kiev amesema madai hayo ya Moscow ni ya uwongo.

Amesema taarifa hizo haziendani na ukweli wa hali ilivyo. Watalaamu huru hatahivyo wameonya kuwa uvamizi wa Urusi katika mkoa huo ni jambo linalowezekana. Mji Mkuu wa Ukraine, Kiev, Jumapili jioni kwa mara nyingine ulilengwa katika mashambulizi makubwa ya droni kutoka Urusi. Hakukuwa na ripoti zozote za uharibifu uliotokea au za vifo na majeruhi.

Wakati huo huo, pande hizo mbili zimelaumiana kuhusu masuala yanayohusu makubaliano ya kubadilishana wafungwa na kurejeshwa kwa askari waliofariki. Kiev ilipuuzilia mbali madai ya Moscow kwamba inachelewesha kurejeshwa kutoka Urusi kwa wanajeshi wa Ukraine waliouawa vitani. Mkuu wa idara ya upelelezi ya Ukraine, Kyrylo Budanov amesema utaratibu huo utaanza wiki ijayo kama ilivyofikiwa katika mazungumzo ya moja kwa moja ya Instabul.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *