
Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi Sergei Shoigu amewasili Pyongyang ambapo atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, mashirika ya habari ya Urusi Tass na RIA Novosti yameripoti leo Ijumaa, Machi 21. Pyongyang imeshutumiwa kwa kutuma wanajeshi katika eneo la Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Korea Kaskazini na Urusi zimeimarisha ushirikiano wao wa kijeshi katika miezi ya hivi karibuni. Nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya ulinzi wa pande zote mbili, na Pyongyang imeshutumiwa na nchi za Magharibi kwa kutuma wanajeshi kupigana katika eneo la Ukraine pamoja na jeshi la Urusi.
Pyongyang imeshutumiwa na nchi za Magharibi na Korea Kusini kwa kutuma wanajeshi kwenye mstari wa mbele nchini Ukraine Ukraine kusaidia jeshi la Urusi, lakini haijawahi kuthibitisha kutumwa kwa wanajshi wake, wala Moscow haijathibitisha.
Kulingana na shirika la habari la Tass, Shoigu, waziri wa zamani wa ulinzi, ameanza ziara yake kwa kuweka shada la maua kwenye mnara wa wanajeshi wa Jeshi Nyekundu waliokomboa eneo la kaskazini mwa rasi ya Korea kutoka mikononi mwa jeshi la Japani mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia.