
Siku moja bada ya mazungumzo kati ya ujumbe wa Marekani na ule wa Ukraine, Kremlin imejibu pendekezo la usitishwaji mapigano wa siku thelathini lililoafikiwa siku ya Jumanne, Machi 11, huko Saudi Arabia kati ya Kyiv na Washington.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Mamlaka ya Urusi haikatai chochote, lakini inangojea kufahamishwa na mshirika wake Marekani juu ya maelezo sahihi na njia za kutekeleza usitishaji huu wa mapigano.
Kwa hiyo Moscow inatoa hisia ya kutaka kupata muda kwa kuendelea kuwafukuza wanajeshi wa Ukraine kutoka katika eneo lake katika eneo la mpaka la Kursk.
Hadi sasa, Vladimir Putin amekuwa akipinga usitishaji mapigano kwa muda. Anataka kufikia kukomesha kabisa kwa mapigano kwa msingi wa maeneo yaliyotekwa na vikosi vya Urusi na kuhitimisha kile anachokiita amani ya muda mrefu, kwa kuzingatia kuheshimu masilahi halali ya wakaazi wote na watu wanaoishi katika mkoa huo.
Mazungumzo yanayowezekana kati ya Putin na Trump
Rais wa Urusi anasema usitishwaji mapigano ungetoa ahueni kuruhusu wanajeshi wa Ukraine kujipanga upya na kuchukuwa tena silaha ili hatimaye kuanzisha tena mzozo. Kwa hivyo, msemaji wa Kremlin amefafanua kuwa ni mapema mno kwa Moscow kufanya uamuzi juu ya pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 30. Kulingana na Dmitry Peskov, wajumbe wa Marekani Marco Rubio na Mike Waltz watafahamisha mamlaka ya Urusi kuhusu maudhui sahihi na maelezo ya makubaliano hayo.
Majadiliano yanatarajiwa kufanyika katika saa zijazo. Na Dmitry Peskov hauondoi uwezekano kwamba Vladimir Putin na Donald Trump wanaweza kuzungumza moja kwa moja, na hata ndani ya “muda mfupi” ikiwa hali inahitaji. Hapo ndipo tutajua iwapo Donald Trump ameweza kukubali msimamo wa Vladimir Putin.
China “yakubali”
Washirika wa Magharibi wa Ukraine wameitaka Urusi kuzungumza. “Mpira sasa uko kwenye uwanja wa Putin,” Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X Mapema Siku ya Jumanne jioni, maafisa wakuu wawili wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, walikaribisha makubaliano hayo na kusema kwamba uamuzi kutoka kwa kiongozi wa Urusi sasa unatarajiwa. China, ambayo inajionyesha kama upande usioegemea upande wowote katika mzozo huo, imesema leo Jumatano kwamba “inaunga mkono” pendekezo la kusitisha mapigano.
Kwa vyovyote vile, washirika wa Ulaya “itabidi wahusishwe,” Rubio amewaambia waandishi wa habari kuhusu nchi za Ulaya wakati wa ziara yake ya kiufundi huko Ireland, akiongeza kuwa Urusi itaomba kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi yake tangu kuanza kwa vita zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Kutokuaminiana
Baada ya mkutano wa Ukraine na Marekani, baadhi ya wanajeshi wa Ukraine walioko mashariki wanapata ugumu kuamini katika mapendekezo ya usitishaji mapigano au wanahofu kwamba yatamfaidi adui wa Urusi. Urusi itakubali makubaliano ya usitishwaji mapigano, lakini haitayaheshimu”,nina uhakika wa 100%,” afisa aliyepewa jina la kivita “Malchik” ameliiambia shirika la habari la AFP. Mjini Kyiv, pendekezo la Marekani pia limepata hisia tofauti: “Kwa kuzingatia hali ya hivi majuzi ya kisiasa nchini Ukraine, sidhani kama usitishwaji mapigano wa siku 30 utasaidia kuleta amani,” Oksana Evsukova, mwalimu, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.