
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema siku ya Alhamisi kwamba ushuru mpya uliotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump ni “pigo kubwa” kwa uchumi wa dunia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Akisikitishwa sana na uamuzi huu, amebainisha kwamba nchi za Ulaya zilikuwa “tayari kuguswa” na zilikuwa tayari zinashughulikia “kifurushi kipya cha hatua za kujibu” ikiwa mazungumzo na serikali ya Marekani, ambayo yalitakiwa sana na Umoja wa Ulaya, EU, yatashindwa.
“Hatujachelewa kushughulikia wasiwasi kupitia mazungumzo.” Ushuru huo mpya ni “pigo gumu” kwa uchumi wa dunia, lakini Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ameweka mlango wazi siku ya Alhamisi, Aprili 3, kwa majadiliano na utawala wa Marekani kuhusu ushuru uliotangazwa na Donald Trump siku ya Jumatano.
Amesisitiza kuwa Kamishna wa Biashara wa Ulaya, Maros Sefcovic, amekuwa “akiwasiliana mara kwa mara” na wenzake wa Marekani. “Tutajitahidi kupunguza vikwazo, sio kuviongeza,” amehakikisha Rais wa Tume ya Ulaya, kutoka Samarkand, Uzbekistan, ambako anashiriki katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya-Asia ya Kati.
“Tangu mwanzo, tumekuwa tayari kufanya mazungumzo na Marekani ili kuondoa vikwazo vilivyosalia kwenye biashara ya Bahari ya Atlantiki. Wakati huo huo, tuko tayari kujibu,” ameonya. Katika hali isiyo ya kawaida, Rais wa Tume ya Ulaya ametoa hotuba yake mara tatu mfululizo, katika lugha tatu: Kiingereza, Kifaransa, na kisha Kijerumani.
Ushuru huo mpya ni “pigo kubwa” kwa uchumi wa dunia, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema mapema siku ya Alhamisi asubuhi.
Nchi za Ulaya “ziko tayari kujibu” lakini “hazijachelewa” kufanya mazungumzo, anasema Ursula von der Leyen.
Donald Trump ametangaza ushuru mkubwa wa forodha, haswa dhidi ya Asia na Umoja aw Ulaya, EU. Tangazo la vita vya kibiashara ambalo limezua hisia kubwa kote duniani na kuutumbukiza uchumi wa dunia katika hali ya sintofahamu.
Donald Trump alianzisha mashambulizi makubwa ya kibiashara Jumatano, Aprili 2, 2025, kwa kutangaza ushuru mkubwa wa forodha, hasa dhidi ya Asia na Umoja wa Ulaya, huku kukiwa na hatari ya kudhoofisha uchumi wa dunia, lakini pia ule wa Marekani. Rais wa Marekani anaona kuwa ni “tangazo la uhuru wa kiuchumi.”