Urithi wa Mashahidi wa Brigedi za Qassam utatokomeza saratani ya Israeli

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema urithi adhimu wa Mashahidi wa Brigedi za Izzudin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, katika vita dhidi ya Israel utatia nuru kwenye mustakbali wa Muqawama.