Upotoshaji mkubwa! Al Jazeera yaficha shukrani za msemaji wa Hamas kwa Iran

Kitengo cha “habari za punde” cha televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwenye mitandao ya kijamii, katika hatua ya kushangaza, kimechuja shukrani zilizotolewa na Obaida, msemaji wa “Brigedi za Izzuddin al-Qassam,” tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kwa Iran na Yemen.