
Upinzani nchini Sudan Kusini umewashtumu wanajeshi wa serikali kwa kushambulia ngome yake, karibu na jiji kuu Juba, siku ya Jumanne, hali inayoendelea kutikisa mkataba wa amani wa mwaka 2018.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la serikali limeripotiwa kuwashambulia vikosi vya Makamu wa kwanza na rais Riek Machar, katika jimbo jirani la Equatoria ya Kati, wakati huu kiongozi huyo akiwa bado anazuiwa nyumbani kwake.
Lam Paul Gabriel, msemaji wa vikosi vya upinzani, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema vikosi vya serikali vilishambulia ngome yake ya Panyume na kusababisha makabiliano makali.
Haijabainika, makabiliano hayo yamesababisha madhara kiasi gani, lakini ripoti zinasema makaazi ya watu na serikali, yameharibiwa vibaya.
Hii ni inakuja, siku mmoja baada ya serikali kusema vikosi vyake kwa sasa vinadhibiti mji wa Nasir, ngome nyingine ya vikosi vya upinzani, katika jimbo la upper Nile.