Upepo wa kisulisuli ulivyopita na mastaa hawa

Dar es Salaam. Kuwa namba moja ni jambo gumu, lakini kuendelea kuwa namba moja ni jambo guu zaidi, wahenga walisema.

Hii iko katika kusaka mafanikio ya maisha ya kawaida na hata katika mambo mengine yote ikiwamo muziki.

Mwananchi limekuchambulia baadhi ya nyota ambao walionekana wanaweza kuleta mapinduzi kwenye tasnia hiyo kutokana na uwezo wao, lakini ghafla wakatoweka!

WAP 01

Recho Kizunguzungu

Ni kipaji kilichokulia na kukuzwa Tanzania House of Talent (THT) walikopita mastaa wengine wa kike kama Nandy, Maua Sama na Ruby.

Alipita kwenye mikono ya aliyekuwa Mkurugenzi wa THT, marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliamini nje ya uwezo wa kuigiza kwa mwanadada huyo kuna kitu kingine cha kuimba ambacho ningempa umaarufu mkubwa nchini.

Wimbo wa kwanza uliompa umaarufu mkubwa Recho ‘Kizunguzungu’ aliutoa mwaka 2011 alipoanza kupata mashabiki mbalimbali kwenye muziki wake.

Nyimbo kama Upepo (2012) na Nashukuru Umerudi (2013) ni kati ya ngoma zilizoendelea kumpa umaarufu mkubwa kwenye kiwanda cha burudani akitabiriwa kuja kuwa Ray C mpya akifanana na mkongwe huyo kwa mengi.

Mara ya mwisho msanii huyo kutoa wimbo, ni miezi minane iliyopita ‘Saizi Yangu’ akimshirikisha rapa, Stamina wimbo uliopata zaidi ya watazamaji 50,000 kwenye mtandao wa YouTube.

Mkali huyo wa kibao cha ‘Umebadilika’ alichomshirikisha Nandy alikuwa tishio kwenye muziki wa Bongo Fleva kutokana na ngoma alizokuwa anatoa.

Alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wanafuatiliwa kutokana na ngoma zake zilizojaa mafunzo na uwezo mzuri wa kupangilia mashairi yake.

Alianza sanaa yake miaka minane iliyopita lakini alikuja vizuri kiasi cha kutabiriwa makubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Ngoma kama ‘Nitunzie’ aliyomshirikisha Barakah The Prince, ‘Mazonge’ aliyofanya na  Jolie na Sina ni kati ya nyimbo zilizofanya vizuri na kumpa umaarufu mkubwa.

Sasa bado anafanya muziki lakini hapewi sikio kubwa na mashabiki.

WAP 02

Hanstone 

Huwezi kuutaja wimbo wa Iokote kutoka kwa msanii Maua Sama bila kutaja jina la mwandishi, Hanstone ambaye alishirikishwa kwenye wimbo wa mwanadada huyo.

Wimbo huo ambao ulitoka miaka sita iliyopita ukipata zaidi ya watazamaji milioni 30 kule YouTube ulimpa umaarufu mkubwa Hanstone ambaye hakuwa nao.

Kitendo cha Maua Sama kumtaja mtunzi wa wimbo huo kilimpa mafanikio makubwa kwenye sanaa yake na kutajwa kama msanii ambaye angeleta mapinduzi makubwa kwenye muziki huo.

Alikuwa anatajwa kuwa mmoja wa wasanii ambao wangesainiwa na lebo ya Wasafi chini Diamond Platnumz, hata hivyo mambo yakavurugika.

Tangu hapo Hanstone alitoa ngoma kadhaa Nimechoka, Yataniua, Acha Lipite na Washamba lakini hazikutoboa akionekana kama hayupo kwenye gemu.

WAP 03

Mwaka 2021 Mac Voice alisainiwa na lebo ya Next Level Music chini ya Rayvanny aliyekuwa anasimamiwa na Lebo ya Wasafi na baadaye kuachana nao. Hakukawia baada ya kusainiwa akatoa EP yake ya kwanza ikienda kwa jina la ‘My Voice’ ikiwa na nyimbo saba na moja alimshirikisha bosi wake ‘Tamu’.

Alitabiriwa kuwa mmoja wa wasanii ambao wangemshusha Rayvanny ambaye ni bosi wake kutokana na juhudi alizokuwa anazifanya ikiwamo kutoa ngoma na kufanya shoo.

Unakwenda mwaka sasa nyota huyo hajatoa ngoma wala kusikika kwenye majukwaa makubwa na wimbo wake wa mwisho ni ‘Mapenzi na Pesa’ aliomshirikisha msanii wa singeli, Meja Kunta.

Bado yupo kwenye lebo hiyo lakini hasikikii.

Wakati anasajiliwa ndio muda ambao Harmonize alimtambulisha Ibraah ambaye kwa sasa anafanya vizuri kama Zuchu wa Wasafi aliyeleta ushindani kwa kinadada.

WAP 04

Ibra Nation 

Achilia mbali ubora wa uandishi wake wa mashairi lakini ni mmoja wa wasanii ambao walikuja vizuri na baadaye wakapotea.

Kwa kuthibitisha ubora wa uandishi wake amewaandikia wasanii wengi lakini ngoma zake kama Nieleze, Naamini na Wangapi zinaendelea kujitafuta.

WAP 05

Benson Hauzimi 

Ni zao la THT na Hauzimi ni wimbo uliomtambulisha Benson kwenye muziki wa Bongo Fleva lakini hakuwa na muendelezo baada ya hapo.

Ni miongoni mwa wasanii wachache waliowahi kuwaandikia wasanii kama Mwasiti na Nandy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *