Uongozi wa Imam Khomeini (RA) na athari zake katika kufanikiwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Karibuni wapendwa wasikilizaji wa Radio Tehran katika mfululizo wa vipindi vyetu vya Alfajiri Kumi na hiki ni kipindi chetu cha kwanza katika kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.