UNRWA: Ukingo wa Magharibi ni ‘uwanja wa vita’, watu 50 wameuawa

Wiki kadhaa za uvamizi wa kijeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu zimegeuza jamii za Wapalestina kuwa “uwanja wa vita” na kuwaacha watu 40,000 bila makazi, mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yameonya jana Februari 26, 2025.