United yamaliza ya tatu Europa, yafuzu 16 Bora

Manchester, England. Manchester United imeonyesha kiwango cha juu na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FCSB kwenye mchezo mkali wa Europa.

Huu ulikuwa mchezo wa mwisho wa hatua ya kwanza kwenye michuano hiyo na kuifanya Man United kumaliza kwenye nafasi ya tatu katika msimamo huo wa timu 36.

Pamoja na United kushindwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye Ligi Kuu England, huku timu hiyo imekuwa ikionyesha uwezo mkubwa uwanjani ikiwa imeshinda michezo mitano na kutoka sare mitatu bila kupoteza mecho yoyote.

Katika mchezo wa jana United ilijipatia mabao yake kupitia Diogo Dalot na Kobbie Mainoo na kuifanya timu hiyo itoke nchini Romania na ushindi huo mnono.

Sasa ni rasmi kuwa United imefuzu kwa hatua 16 kati ya zile nane za kwanza na sasa kutakuwa na mechi za mtoano ambapo timu kuanzia nafasi ya tisa hadi nafasi ya 24 zitapambana kwenye mechi za mtoano kupata timu nane nyingine.

Kwa upande wa Tottenham iliyomaliza nafasi ya nne kwenye msimamo ilifanikiwa kuichapa Elfsborg mabao 3-0 na kufikisha pointi 17 kwenye michezo nane iliyocheza msimu huu kwa mabao yaliyofungwa na Dane Scarlett, Oyindamalo Ajayi na Mikey Moore.

Zilizofuzu

Timu nane ambazo zimefuzu moja kwa moja baada ya michezo ya jana ni Lazio ambayo imemaliza kileleni, Athletic Club iliyomaliza nafasi ya pili, Man United, Tottenham Hotspur, Frankfurt pamoja na Rangers.

Zinazocheza mtoano

Bodo, Andelecht, FCSB, Ajax, Real Sociedad, Galatasaray, Roma, Vicktoria Plzen, Frencvaros, Porto, Az Akmaar, Midtjylland, Union, Poak, Twente na Fernabahce