UNICEF yapokea dola milioni 1.5 za kuwasaidia watoto wakimbizi wa Sudan walioko Libya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilisema jana kwamba limepokea msaada wa dola milioni 1.5 kutoka kwa Shirika la Education Cannot Wait (ECW) ambao ni mfuko wa Umoja wa Mataifa wa elimu katika dharura. Msaada huo utatumika kushughulikia mahitaji ya dharura ya kielimu na kisaikolojia ya watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Libya.