UNHCR: Tunahitaji dola milioni 40 kusaidia wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Wakati waasi wa M23 wakiendelea kusonga mbele katika mkoa wa Kivu Kaskazini na Kusini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeaomba zaidi ya dola milioni 40 kusaidia watu waliokimbia makazi yao katika mikoa hiyo mawili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na katika nchi jirani.