Unajua tabia ulizonazo zinatokana na kundi lako la damu?

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A, B, AB na O.

Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yanaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya.

 Wataalamu wanasema tabia ya mtu na uhusiano na kundi la damu alilopo,  ni  jambo la uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine.

Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea, kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula.

Baadhi ya watafiti wa Kikorea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kukaa, hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu.

Damu kundi  A

Hawa watu mara nyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwa sababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema, wapole na wenye tabia njema.

Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo  na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.

Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika  na kubeba majukumu yao, wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu na wenye tabia njema.

Kwa upande wa upungufu wao,  ni wasumbufu, wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu, wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.

Katika maisha yaa kijamii, ni watu unaoweza kuwaamini na kuwategemea, wanajali na kumaanisha. Wakati wote huepuka shari, misuguano na ugomvi. Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu, wanapendelea ukimya na utulivu.

Kazini, unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu, wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.

Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo na hii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi. Wasiowaelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi.

Kwenye uhusiano na mapenzi, ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.

Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneo ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.

Sifa nyingine za watu hawa, ni  wabunifu na wenye ujuzi wa usanii. Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana. Wengi wao hupendelea kula mboga mboga.

Damu kundi “B”

Watu wa kundi hili mara nyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wana ndoto na maono makubwa, wanasukumwa kwa kasi na kiu zao, ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao.

Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata kama ulimwengu mzima usimame kinyume nao.

Wanasukumwa  katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji, wanapenda raha, wana hisia nzito, wanayatazama maisha katika mtazamo chanya, wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.

Udhaifu wao ni pamoja na ubinafsi sana, mara nyingine wanakwepa majukumu yao, wagumu sana kusamehe, wasumbufu, wanaweza kuwa katili na wenye hasira za haraka.

Kijamii, mara nyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao,  maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.

Kazini,   wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya peke yao.

Kimapenzi, unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia, fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, katili na wasioaanisha kile wanachokisema.

Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao.

Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.

Sifa nyingine,  wana tabia ya utukutu, kupenda  wanyama, wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa. Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maziwa.

Damu kundi   “AB”

Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko; hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga,  wenye aibu, wengine ni wapenda mitoko na wacheshi.

Wako wanaofanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanachotaka kukifanya. Hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza  unapokuwa nao.

Uzuri wao ni rahisi sana kuwa rafiki nao, wanaendana  na mazingira haraka na kwa urahisi, wafurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.Wana mawazo, wana akili sana, hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.

Kasoro zao ni wagumu katika kufanya uamuzi, wanasahau sana. Ni wenye hisia za kuyumba “mood swing”, yaani mara wana furaha mara wamekasirika. Sio waaminifu, ni wapinzani, wabishi, wakosaji na wanapenda ubinafsi.

Kijamii, wanaweza  kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.Maongezi yao ni yenye kuhamasisha na yenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.

Kazini, wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao,  lakini sio watu wa kuwategemea sana, kwani wanaweza kukuangusha kirahisi.

Kiuhusiano, kuwa katika uhusiano na mtu wa kundi la damu la AB,  kunaweza kuwa kwenye kufurahisha, unaweza usiwe na nyakati nyingi za upweke.

Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na mara nyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi,  lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara, na pale inapobidi,  basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.

Sifa zao nyingine, ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha. Maranyingi wanajihusisha na kupendelea shughuli za kisanaa au mambo yenye sanaa.

Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu, watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.

Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’, watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga  na pia vyakula vitokanavyo na wanyama.

Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine.

Wana  moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana na ya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao, ni watu wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi  mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidii, ni waaminifu, wanaweza kujieleza.

Ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuona mambo hata kabla hayajatokea, wana kiu ya kufahamu na kudadisi na pia ni watu wema na watoaji.

Shida yao  wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu. Unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na ni rahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya.

Kwenye maisha ya kijamii, ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea,; ni waaminifu, ni wawazi, ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi. Pia  wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.

Kazini, wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa hukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo,  ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayofanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe.

Kuhusu mapenzi, ni watu wanaoweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda,  ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.

Sifa zao nyingine, wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama.

 Dr. Chris Mauki

Social, relationship and counseling psychologist

University of Dar es salaam