UN yatoa wito wa karibu dola bilioni 1 kwa ajili ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladeshi

Umoja wa Mataifa na washirika wake wametoa wito Jumatatu, Machi 24, wa karibu dola bilioni 1 kutoa msaada muhimu kwa wakimbizi wa Rohingya milioni 1.5 nchini Bangladeshi na kwa nchi inayowapokea.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa na zaidi ya washirika 100 wamezindua Mpango wa Majibu ya Pamoja 2025-26 ili kukabiliana na mzozo mkubwa unaowakumba wakimbizi wa Rohingya, na wanaomba “dola milioni 934.5 katika mwaka wake wa kwanza kufikia takriban watu milioni 1.48, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Rohingya na jumuiya zinazowahifadhi,” taarifa hiyo imesema.

Mapema mwezi huu wa Machi Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada endelevu wa kifedha kwa wakimbizi wa Rohingya wanaoishi katika mazingira magumu sana nchini Bangladeshi.

Kulingana na Filippo Grandi, wako hatarini kukumbwa na majanga ya asili na wanategemea takriban misaada ya kibinadamu kukidhi mahitaji yao ya kimsingi.

“Iwapo misaada ya kimataifa itapungua kwa kiasi kikubwa – jambo ambalo lina uwezekano wa kutokea – kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Bangladesh, mashirika ya misaada na wakimbizi wenyewe itaathiriwa pakubwa, na kusababisha maelfu ya watu kukumbwa na njaa, magonjwa na ukosefu wa usalama,” mkuu wa UNHCR alisema wakati akihitimisha ziara ya siku nne nchini humo Bangladesh.

Huko Cox’s Bazar, Bwana Grandi alizungumza na wakimbizi waliowasili hivi karibuni katika kambi hizo baada ya kukimbia ghasia zinazoendelea katika Jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Mzozo mkali  katika Cox’s Bazar siku za hivi karibuni umezidisha hali mbaya ya warohingya, na wengi hawakuwa na chaguo ila kuhatarisha maisha yao kwa kulazimika kukimbilia nchini Bangladeshi kutafuta usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *