
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza Ijumaa, Machi 28, kushuka kwa asilimia 40 ya ufadhili wake kwa mwaka 2025, likitaja “mgogoro ambao haujawahi kutokea” huku watu milioni 58 wakiwa katika hatari ya kupoteza misaada muhimu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Kwa sasa, shirika linakabiliwa na kushuka kwa hali ya kutisha kwa asilimia 40 ya ufadhili kwa mwaka 2025, ikilinganishwa na mwaka jana.” “Ukali wa upunguzaji huu, pamoja na rekodi ya idadi ya watu wanaohitaji, imesababisha mgogoro usio na kifani kwa makumi ya mamilioni ya watu duniani kote,” WFP imesema katika taarifa.
Shirika hilo linakumbusha kuwa “linatoa kipaumbele kwa nchi zenye mahitaji makubwa.” “Pamoja na kwamba tunafanya kila tuwezalo kupunguza gharama za uendeshaji, hatupaswi kudanganywa, tunakabiliwa na pengola fedha ambalo matokeo yake yanaweza kuwa mabaya,” ameonya Rania Dagash-Kamara, mkuu wa ushirikiano na uvumbuzi wa WFP.
Huko Gaza, msaada wa chakula utaisha ndani ya siku 15 Kulingana na makadirio ya WFP, “watu milioni 58 wako katika hatari ya kupoteza msaada wa kuokoa maisha kutokana na oparesheni 28 muhimu zaidi za shirika hili kutokana na uhaba wa fedha.” Tayari WFP ilikuwa imeonya siku ya Alhamisi kwamba imebakiwa na wiki mbili pekee za msaada wa chakula huko Gaza na njaa inatishia tena, tangu kuanza kwa operesheni za kijeshi za Israel katika ardhi ya Palestina.
Matangazo ya kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni, na kuzua wasiwasi miongoni mwa mashirika yasito ya kiserikali na mashirika ya kimataifa. Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa hivyo umeondoa 83% ya programu za shirika la maendeleo la Marekani USAID, linalowakilisha “makumi ya mabilioni ya dola” ya msaada kwa WFP. USAID pekee ilisimamia bajeti ya kila mwaka ya dola Bilioni 42.8, au 42% ya misaada ya kibinadamu iliyotolewa duniani kote. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pia zimepunguza bajeti zao za misaada ya kimataifa, kama zilivyofanya nchi za Skandinavia.