UN yatahadharisha mauaji ya kimbari ya Israel yanaweza kupanuka hadi Ukingo wa Magharibi

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika ardhi za Palestina ametahadharisha kuwa mauaji ya kimbari ya Israel yanaweza kupanuka kutoka Gaza hadi Ukingo wa Magharibi, kwa kuzingatia operesheni kubwa ya kijeshi inayoendelea kufanywa na utawala huo ghasibu katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Jenin.