UN yalaani mashambulizi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi na kuutaka utawala huo kusitisha mara moja “wimbi la tahadhari ya machafuko na ukimbizi wa umati” kwa raia wa Palestina.