UN: Pande mbili za vita vya wenyewe kwa wenyewe Kongo DR vinafanya mauaji, ubakaji

Umoja wa Mataifa umezishutumu pande mbili za vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa zinahusika na mauaji ya watu wengi na ubakaji, huku waasi wanaoungwa mkono na Rwanda wakizidi kusonga mbele katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini kama vile almasi, dhahabu, shaba na yale ya coltan yanayotumika katika simu za mkononi.