UN: Mbali na hatari za kiusalama, afya za watu wa Goma pia zinahatarishwa na magonjwa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, wakati huu ambapo hatari za kiusalama zimeanza kupungua na utulivu umeanza kurejea huko Goma ambao ni mji mkubwa zaidi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), afya za wakazi za mji huo ziko kwenye hatari ya kukumbwa na miripuko ya magonjwa kama kipindupindu na Mpox.