UN: Mashambulizi ya Israel yamepelekea Wapalestina 40,000 kupoteza makazi

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema kuwa uvamizi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi umesababisha “uhamishaji mkubwa wa watu” ambao haujawahi kushuhudiwa tangu vita vya mwaka 1967, vilivyosababisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.