UN: Maelfu ya raia Kongo wahama makazi yao baada ya M23 kutoa muhula wa masaa 72

Waasi wa M23 wanaodhibiti miji ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefunga kwa nguvu kambi za makazi za raia na kuwalazimisha zaidi ya watu 110,000 kuhama makazi yao katika siku za hivi karibuni. Haya yameelezwa na Umoja wa Mataifa.