UN inataka Dolla Milioni 11.2 kuisaidia Uganda kupambana na Ebola

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa dharura wa kuchangisha dola milioni 11.2 kusaidia Uganda kukabiliana na mlipuko wa Ebola ambao umesababisha vifo vya watu wawili, baada ya bajeti ya afya ya nchi hiyo kudhoofishwa kutokana na hatuaj ya Marekani kusitisha misaada ya nje.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Uganda ilitangaza kuzuka kwa ugonjwa huo mwezi Januari katika mji mkuu wa Kampala baada ya kifo cha muuguzi wa kiume wa hospitali ya rufaa ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mgonjwa wa pili wa Ebola, mtoto wa miaka minne, alifariki wiki iliyopita, limesema Shirika la Afya duniani, likinukuu wizara ya afya ya nchi hiyo.

Wagonjwa 10 waliothibitishwa nchini Uganda wamehusishwa na ugonjwa wa Ebola nchini Sudan ambao hauna chanjo iliyoidhinishwa.

Katika taarifa iliyotolewa hapo jana, Umoja wa Mataifa unasema fedha hizo zitagharamia operesheni za kukabiliana na virusi hivyo kuanzia Machi hadi Mei katika wilaya saba zilizo katika hatari kubwa.

Uganda imekuwa ikitegemea Marekani kwa ufadhili katika sekta yake ya afya.

Wakati wa mlipuko wa mwisho wa Ebola mwaka 2022-2023, Marekani ilitoa dola milioni 34 kufadhili udhibiti, ufuatiliaji, uchunguzi, maabara miongoni mwa shughuli nyingine, kulingana na ripoti ya Ubalozi wa Marekani.