
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limesema siku ya Jumatatu linahitaji dola milioni 19.8 kwa dharura kulisha wakimbizi 120,000 ambao wamekimbia mzozo wa DR Congo na ambao kwa sasa wako nchi jirani ya Burundi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema watu 70,000 wamekimbilia Burundi tangu mwezi Januari baada ya kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda kuteka maeneo makubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hiyo imefanya jumla ya watu wanaohitaji msaada wa chakula nchini Burundi kufikia 120,000, WFP imesema.
“Wakimbizi wanawasili kila siku, wengine wakiwa wamebeba mabunda na masanduku kwa yaliyojaa vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na guo, na wengine wakiwa hawana chochote ila nguo mgongoni,” Dragica Pajevic, naibu mkurugenzi wa WFP kanda ya Afrika Mashariki, amesema katika taarifa.
“Ingawa tunashukuru kwa ufadhili uliotolewa hadi sasa, lakini hautoshi. Rasilimali zetu zilizopo zinatumiwa zaidi ya uwezo wetu, na tunalazimika kurekebisha shughuli zetu na kupunguza mgao,” Pajevic ameongeza.
WFP hutoa chakula kwa wakimbizi walio katika kambi za muda, kama vile shule, makanisa na viwanja vya michezo.
Imesema imelazimika kupunguza mgao kwa nusu kwa wakimbizi waliopo ili kuhudumia wimbi hilola wakimbizi.
Bila ufadhili wa ziada, shirika hilo linasema litalazimika kusimamisha msaada wa chakula kabisa ifikapo mwezi Julai.
WFP imeomba dola milioni 19.8 ili kudumisha usaidizi hadi mwisho wa mwaka.