UN: Hofu ya magonjwa ya miripuko yatanda katika mji wa Goma unaokaliwa kwa mabavu

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Goma wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaokaliwa kwa mabavu, alisema jana Jumatano kuwa mji huo uko katika hali mbaya huku wasaidizi wa masuala ya kibinadamu wakipambana na hatari ya magonjwa ya mripuko.